Baada ya kusomea
taaluma ya Sheria kwa muda mrefu, inanipasa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya
sheria ambayo yanawatatanisha ama hawajapata fursa ya kuzisoma. Mwanzo,
mtaniruhusu kudurusu vipengele muhimu yanayohusu bunge. Kuelewa bunge ndiko
kuelewa jinsi ambavyo inaendesha masuala yake na matarajio yako mwananchi kwa
wajibu unaomkabidhi kwa kumchagua.
Imenibidi kuwasilisha
ujumbe huu kwa Kiswahili kwa sababu lugha ya mkoloni si wengi wanaizungumza na
kuielewa. Pia, elimu kwa umma inapaswa kuwa kwa lugha inayoeleweka kwa urahisi.
Muhtasari:
Katiba ya Jamhuri ya
Kenya inazungumzia suala la Bunge katika Sura
ya nane kuanzia kipengee cha 93
hadi 128. Imegawanywa katika sehemu
sita.
Sehemu
mbali mbali
Sehemu
ya Kwanza— Kuundwa na jukumu la Bunge
Sehemu
ya Pili— Wanachama wa Bunge
Sehemu
ya Tatu— Maafisa wa Bunge
Sehemu
ya Nne— Taratibu za kupitisha sheria
Sehemu
ya Tano—Taratibu na sheria za Bunge
Sehemu
ya Sita- Ziada
Haya basi twende moja
kwa moja hadi Sura ya Nane.
~
SURA
YA NANE
BUNGE
Kuundwa
kwa Bunge
93. (1) Kuna Bunge buniwa la Kenya
litakalojumuisha Bunge na Seneti.
(2)
Bunge na Seneti zitatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba hii.
Jukumu
la Bunge
94. (1) Jukumu la kutunga sheria la Jamhuri
hii katika kiwango cha kitaifa ni la Bunge.
(2)
Bunge hutokeza tofauti za kitamaduni katika taifa, linawakilisha maoni ya
watu
na hutekeleza mamlaka yake.
……
Jukumu
la Bunge
95.
(1) Bunge linawakilisha watu wa maeneo
bunge na matakwa muhimu katika Bunge.
(2) Bunge lina uwezo wa kupitisha
sheria kulingana na sehemu ya 4 katika sura hii.
(4) Bunge lina jukumu la—
(a)
kuidhinisha kugawana kwa mapato
miongoni mwa viwango mbalimbali vya serikali na miongoni mwa serikali zenyewe
katika kila kiwango na kukadiria hazina ya gharama ya serikali ya kitaifa na
taasisi nyingine za Serikali ya kitaifa kwa mujibu wa Sura ya Kumi na Mbili;
(b)
kutenga fedha za matumizi za serikali ya Kitaifa na sasi zingine za Taifa;
(c) kufuatilia kuona iwapo kumekuwa uwazi
katika matumizi ya rasilmali za kitaifa.
(5) Bunge lina jukumu la—
(a)
kuchunguza utendakazi wa ofisi ya Rais, Naibu wa Rais na maofisa wa Serikali na
ikiwezekana kuanzisha hatua za kuwatoa ofisini; na
(b)
kuchunguza kwa makini na kusimamia hatua zinazochukuliwa na taasisi za
Serikali.
(6)
Bunge lina mamlaka ya kuidhinisha matangazo ya vita na kuendelezwa kwa tangazo
la muda wa hali ya hatari.
Jukumu la Seneti
96. (1) Seneti linawakilisha kaunti, na litashughulikia masuala ya kaunti za
serikali zao.
(2) Seneti litashiriki katika kukusanya
na kutunga sheria ya kitaifa na kulinda maslahi ya serikali hiyo iliyogatuliwa
kwa mujibu wa vipengee vya 109 hadi 113.
(3) Seneti litashughulika na kutenga
fedha za matumizi za serikali ya Kitaifa katika serikali iliyogatuliwa kwa
mujibu wa kipengee cha 217, na kuchunguza kwa makini matumizi za pesa za
serikali.
(4) Seneti litajishirikisha katika uchunguzi wa makini wa Maafisa wa
Serikali, kuchunguza utendakazi wa ofisi ya Rais au Naibu wa Rais na
ikiwezekana kuanzisha hatua za kuwatoa ofisini kwa mujibu wa kipengee cha 145.
~
Itabidi nikome hapo
kwa leo. Katika makala mengine, nitatathmini vipengele vingine vilivyomo ndani
ya Katiba.
Nikisoma Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Jumuiya ya Tanzania, nimefurahishwa na jinsi ambavyo
wametumia lugha ya Kiswahili haswa katika haya:
i.
Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti
ya ibara hii neno "…." Maana yake ni….
ii.
Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo
ya (1),….
iii.
Ibara kwa kiingereza ni Section.
iv.
Misingi ya Katiba kwa kiingereza ni Preamble.