Waashiki
wa sheria watakubaliana nami kuwa mfumo wa sheria umebadilika kufuatana na
kupitishwa sheria mpya za ardhi.
Rais
aliziidhinisha miswada hii na kuzifanya kuwa sheria tarehe 27 Aprili 2012:
v
Land
Act (No. 6 of 2012);
v
The
Land Registration Act (No. 3 of 2012); na
v
The
National Land Commission Act (No. 5 of 2012).
Sheria za ardhi ambazo zilikuwa
zikitumika hapo awali zilikuwa:
v
The
Registered Lands Act (RLA);
v
The Registration
of Documents Act (RDA);
v
The
Governments Lands Act (GLA);
v
The Indian
Transfer of Property Act (ITPA);
v
The Land
Titles Act (LTA);
v
The
Registration of Titles Act
Baadhi za lawama
ambazo zimekuwa zikilimbikiziwa sheria za ardhi za hapo awali ni kuwa zilikuwa
zimezagaa hivi kwamba aliyetaka kuzichunguza angetatizika. Wanasheria na
mawakili ambao walifaa kutumia fomu na kuandika mikataba ya ardhi hawakufurahia
hali hiyo. Hivyo basi, sheria hizi mpya ni jambo zuri.
Katika makala
yatakayofuata, nitaangazia baadhi za kasoro za sheria hizi mpya na kutoa
ulinganisho na mifumo ya hapo awali.
No comments:
Post a Comment