KAULI MBIU

Hii blogu imezunduliwa upya kwa jina "JUKWAA LA SHERIA" ili kukimu mahitaji ya wengi ambao hawajapata kufahamu katiba na sheria za kenya. Hali hii imechangiwa pakubwa kutokana na lugha ya Kiingereza ambayo haijafikisha ujumbe kwa mwananchi wa kawaida.

Kutokana na ufahamu wangu mdogo wa Kiswahili na ari niliyo nayo kujifunza zaidi, blogu hii itajadili masuala mengi tu ambayo yataelezea sheria kwa urahisi mno ili ieleweke na yeyote yule atakayeisoma.

Mimi ni mwanafunzi wa Sheria. Nimehitimu. Hivi punde nitaapishwa kuwa wakili. Hivi sasa ninajishughulisha sana na masuala ya sheria za bunge Kenya, nimetunga mashairi katika lugha ya kiingereza na natumai kuja kwako hapo itakufaa.

Asante.

No comments:

Post a Comment